Usiumie Wakati Wanakudharau…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Safari ya mafanikio yeyote ile…

…ndani yake huwa kuna wakati wa kudharauriwa.

Ndio, yaani kuna watu watainuka na kudharau safari yako kwa sababu kubwa 3:

Moja, wanaona haufananii na unachokitaka.

Yaani, wakiangalia historia yako, elimu, uwezo wako wa kifedha n.k…

…wanaona hakuna uwezekano wa wewe kupata UNACHOKITAKA.

Hawa wamesahau kuwa, Mungu huwa ana njia za…

…kumuinua mtu kinyume na matarajio ya wanadamu.

Mbili, kuna ambao wanakudharau kwa sababu ya MWANZO WAKO MDOGO.

Yaani, wanaangalia ULIPO sasa hivi na UNAKOTAKA KWENDA wanaona vitu viwili tofauti.

Huwa wanadhania kuwa wale wanaoweza lazima waanze na VINGI.

Tatu, kuna watu wengi HAWAONI kile UNACHOKIONA.

Yaani, wewe unaona KESHO kubwa na una ndoto KUBWA.

Ila wao wamekupimia, wanakuona UKIBAKIA VILEVILE ULIVYO.

Usihangaike na wanaokudharau, usibishane nao.

Pambania ndoto yako.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment