Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tottenham wamemaliza ukame wao wa miaka 17 bila taji baada ya bao la Brennan Johnson katika kipindi cha kwanza kutosha kuwachapa Manchester United kwenye fainali ya Europa Ligi.
Ushindi huo unamaanisha kuwa kocha mkuu anayekabiliwa na shinikizo la kufukuzwa, Ange Postecoglou, ametimiza ahadi ya kuleta taji katika msimu wake wa pili Spurs.

Postecoglou, ambaye alisema “hatawahi kuwa kichekesho” katika hotuba yake kabla ya mechi, alileta tabasamu na furaha isiyo na mipaka kwa mashabiki 15,000 rasmi, na wengi wasio rasmi, wa Tottenham kwenye Uwanja wa San Mames jijini Bilbao.





Ushindi huu huenda usimuokoe Postecoglou kutimuliwa Spurs katika wiki zijazo. Lakini Muaustralia huyo ataondoka kama shujaa baada ya kocha wa tatu pamoja na Bill Nicholson na Keith Burkinshaw kutwaa taji la Uropa akiwa na vigogo hao wa London Kaskazini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.