Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kufichua udhaifu wako.
ii. Kutambulisha watu wapya wenye uwezo mkubwa kwenye kila eneo
iii. Kuleta mfumo mpya wa maisha.
iv. Kudhihirisha nguvu ya Mungu.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Kusudi La Nne
– Kudhihirisha Nguvu Ya Mungu.
Hakuna kitu kingine kinachomrudisha mwanadamu kwa Mungu isipokuwa janga.
Hata wale ambao hawakuwa na muda wa ibada na….
…kuhitaji msaada wa kiMungu wataanza kumuomba Mungu kwenye kipindi hiki cha janga.
Janga ni namna ya kuikumbusha nafsi ya mwanadamu kwamba sisi wanadamu peke yetu hatuwezi.
Ni kwenye kipindi cha janga ambapo watu huwa hawajui nini wafanye.
Na wanaanza kukimbilia kwa viongozi wao wa kisiasa.
Ambapo hugundua kwamba viongozi hao hawana jibu.
Na kwamba wao pia wanatafuta msaada wa Mungu.
Ni rahisi sana kutangaza kujitosheleza kama Taifa.
Au watu binafsi pale mambo yanapokuwa yako sawa.
Ila ni kwenye kipindi cha janga mambo yakiwa magumu.
Na pale ambapo kila mtu hajui afanye nini…
…ndipo watu huanza kutafuta msaada wa kiMungu.
Hata wale ambao wanakiburi na majivuno…
…nguvu ya janga huwanyenyekesha kila mmoja.
Na kugeuza mioyo yao kumwelekea mwenyezi Mungu.
Unakumbuka uliposema huna muda wa kwenda ibadani?
Lakini ulipopokea taarifa mbaya kutoka kwa daktari kila kitu kilibadilika…
…na ukapata muda mwingi wa kumwomba Mungu?
Janga huja kama kengele ya hatari kwenye maisha yetu kwamba peke yetu hatutaweza.
Kumbuka kwamba pale ambapo mioyo na mataifa yatakapomgeukia Mungu kweli kweli na kuliitia jina lake:
Yuko tayari kudhihirisha nguvu yake na kuwapa watu hekima ya namna ya kuibuka washindi.
Usimwekee Mungu mipaka kwenye kile anachoweza kufanya kwenye majira haya, kuzidishwa kutakuja kipindi hiki cha janga.
Acha kuungana na wale wanaosema tunadidimia au wanaosema hakuna jambo litakalofanikiwa kwa sasa.
Tengeneza kesho yako ambayo ni chanya kwa kukiri…
Kwenye kipindi cha hili janga nitazidishwa…
Jina langu litatambulishwa…
Nitapata msaada wa kiungu…
Na Mungu atakuwa upande wangu…
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.