Je wajua-Edwin C. Barnes

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mnamo mwaka 1905 EDWIN C. BARNES aliamua kujitosa na kudandia treni ya mizigo ili kusafiri kwenda West Orange, New Jersey kukutana na THOMAS EDISON mmoja kati ya wavumbuzi wakubwa kuwahi kutokea duniani. Hii ni kufuatia NDOTO yake, KIU yake, NIA na SHAUKU yake kubwa ya kuwa mfanya biashara mwenza (Business Partner) wa Thomas Edison. Edwin Barnes alikuwa na hali duni ya kimaisha, alikuwa na ujuzi na elimu ndogo sana, LAKINI hiyo haikuweza kuzima MOTO uliokuwa ndani yake.

Mbaya zaidi Edwin Barnes hakuwa na sifa wala umaarufu wowote ambao ungemtambulisha kwa Thomas Edison, Wala hakuwa na nauli ya kumfikisha alipo Mvumbuzi Thomas E.

Edwin Barnes aliamua kusafiri kwa treni ya mizigo mpka kwa Thomas Edison. Alipofika alijitambulisha na kujieleza kwa KUJIAMINI, kuwa “Mimi naitwa Edwin C. Barnes, nimekuja hapa kwa lengo na shauku kubwa ya kuwa mfanya biashara mwenza wako”.

Wasaidizi wa Thomas E walipigwa na butwaa na kusisimuka kufuatia, maelezo ya Edwin Barnes kwa Thomas Edison, hasa ukizingatia alioekana mtu alliyechoka kimaisha, duni, na hohehahe. LAKINI, Thomas Edison hakustaajabu wala kucheka, BALI alivutiwa sana na MOYO wa UJASIRI, SHAUKU na NIA YA DHATI kutoka kwake.

Thomas Edison, hakuweza kukubali kirahisi wazo la Edwin Barnes la kuwa mfanyabiashara mwenza, Bali aliamua kumpa ajira ya kufagia Maabara/Karakana yake. Kama ambavyo isingekuwa rahisi kwa mtu mwingine kupokea matokeo ambayo hayakutarajia, Edwin Barnes alikuwa wa tofauti, alipokea kwa furaha na kukubali kufanya kazi hiyo kwa juhudi, huku akiamini kuwa kazi hiyo itafungua MILANGO ya NDOTO KUU ya kufanya biashara na Thomas Edison.

Edwin Barnes alifanya kazi ya kufagia kwa miaka miwili bila kukata tamaa, huku akijifunza kwa making jinsi Thomas anavyofanya kazi zake.Kipindi hicho pia mvumbuzi guru Thomas Edison alikuwa amevumbia na kuunda kifaa chake kilichoitwa, “EDIPHONE” ambacho alitaka kuingiza sokoni rasmi.

Thomas Edison alipowasilisha kwa wasaidizi wake wazo la kuingiza kifaa sokoni, kila mtu aliguna na kukataa huku wakidai kuwa uhitaji wa kifaa hicho kwa watu mdogo na hakitaleta maslahi yeyote kwa kampuni. Hivyo waliamua kupiga chini.

Hapo ndipo, milango ya FURSA ya ndoto kuu ya Edwin Barnes ilipofunguka. Yeye alikuwa na mtazamo Chanya tofauti na wasaidizi wa Thomas Edison. Aliona FURSA kuwa kifaa hicho kina manufaa makubwa kwa watu na kuna uhitaji mkubwa mno. Ndipo alipoandika pendekezo la mchakato wa “Masoko na Uuzaji wa kifaa”, na kuwasilisha kwa Thomas Edison.

Thomas Edison allikubali wazo la Edwin Barnes, na wakaanza kufanya biashara pamoja. Edwin Barnes aliuza vifaa vingi na kusambaza sehemu mbalimbali nchini marekani. Alitengeneza fedha nyingi Sana, mpka baadae akaanzisha kampuni yake iliyoitwa, “Edwin C. Barnes and Brothers”. Nzuri zaidi NDOTO yake kubwa ya kuwa mfanyabiashara mwenza wa Thomas Edison ilitimia. Mwishowe wakaamua kuzindua kauli mbiu yao inayosema, “MADE BY EDISON AND INSTALLED BY BARNES”.

Tunajifunza nini?
1.Usiogope kumfuata mtu ambaye unaamini ana mchango mkubwa katika kutimiza ndoto yako.

2. Anza na ulichonacho kichwani, usisubiri uwe na kila kitu mkononi

3. Kuna mda inabidi ujitose tu na kufanya maamuzi magumu ili kufikia ndoto yako.

4. Kubali kuanzia chini ili uweze kufika juu(Top).

5. Uvumilivu na ustahimilivu ni nguzo kubwa ya kutimiza ndoto yako.

6.Hakuna kisichowezekana.

Wewe umejifunza nini?

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment