Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Epuka msongo wa mawazo unaoweza kuepukika.
ii. Badilisha vitu au hali zinazokusababisha msongo wa mawazo.
iii. Amua kuendana na mazingira.
iv. Kubaliana na hali halisi.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Mbinu Ya Tatu
– Amua kuendana na mazingira.
Kuna vitu huwezi kuvibadilisha wala kuviepuka…
…namna pekee unayoweza kufanya na kukubali kuendana navyo.
Mfano upo kwenye mahusiano, wewe unapenda mpira mwenzio anapenda filamu, kila mtu anakipenda chake.
Ili msiumizane na kuzozana wote mnaweza kuamua kuacha mnavyovipenda…
…na kutafuta kitu kingine ambacho wote mnakifurahia.
Kwa namna hiyo mtakuwa mmekwepa msongo wa mawazo unaosababishwa na tofauti zenu.
Usiwe aina ile ya watu ambao huwa wanasimamia cha kwao tu.
Na wanataka kile ambacho wanakiamini wao ndio kifanyike…
…tena kwa namna wanavyotaka wao.
Ukiwa mtu wa namna hii utasumbuliwa na stress za mara kwa mara.
Kama una bosi wa aina fulani ambaye huwa anakusababishia stress.
Na una mpango wa kuendelea kukaa kwenye ofisi hiyo kwa muda mrefu…
…inamaanisha unatakiwa kutafuta mbinu za kuishi naye hadi pale utakapoamua kuondoka.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.