Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Israel imetangaza kuwa itaruhusu “kiasi cha chakula” kuingia Gaza ili kuhakikisha kuwa “hakuna janga la njaa linaloendelea” baada ya kulizuia eneo hilo kwa wiki 10.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema kuwa hatua hiyo imetolewa kwa mapendekezo ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) na kwa kuzingatia haja ya kuunga mkono mashambulizi yake mapya ya kijeshi dhidi ya Hamas.
Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya jeshi la Israel kusema kuwa limeanza “operesheni kubwa za ardhini” kote Gaza.
Israel imekuwa chini ya shinikizo kubwa la kuondoa kizuizi chake, wakati ambapo hakuna chakula, mafuta au dawa zilizoruhusiwa kuingia.
Mashirika ya misaada yametahadharisha kuhusu hatari ya njaa miongoni mwa wakazi milioni 2.1 wa Gaza, huku picha za video na zikiibuka za watoto waliodhoofika wanaokabiliwa na utapiamlo.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alitoa wito kwa Israel kuruhusu “mara moja, kuanza tena misaada kwa ajili ya Gaza.
Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilisema kuwa Israel itaruhusu “kiasi cha chakula kuletwa kwa ajili ya wakazi” wa Gaza ili “kuhakikisha hakuna mzozo wa njaa unaoendelea” na kuongeza kuwa hali kama hiyo itahatarisha mashambulizi yake mapya, yaliyopewa jina la Operesheni Gideon’s Chariot.
Mapema siku ya Jumapili, IDF ilianzisha mashambulizi katika maeneo ikiwa ni pamoja na hospitali kaskazini mwa Gaza.
Israel inasema inalenga kuwaachia huru mateka wanaoshikiliwa Gaza na kuwashinda Hamas.
Mashambulizi yalipiga mji wa kusini wa Khan Younis, pamoja na miji ya kaskazini mwa Gaza, ikiwa ni pamoja na Beit Lahia na kambi ya wakimbizi ya Jabalia, waokoaji walisema.
Takribani watu 67 wameuawa na 361 kujeruhiwa huko Gaza katika saa 24 zilizopita, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas ilisema.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.