Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Chanzo kikuu cha Hamas kiliiambia BBC Jumapili jioni kwamba “hakuna mafanikio yoyote au maendeleo ambayo yamepatikana kufikia sasa katika mazungumzo yanayoendelea huko Doha kutokana na kuendelea kuasi Israel”.
Chanzo hicho kilisema Hamas imeonesha nia ya kuwaachilia mateka wote wa Israel kwa awamu moja, “kwa sharti la kufikia makubaliano ya kina na ya kudumu ya kusitisha mapigano , jambo ambalo upande wa Israel unaendelea kukataa, kwani timu yao ya mazungumzo haina mamlaka ya kuamua juu ya masuala muhimu”.
“Israel inazuia fursa yoyote ya kufikia makubaliano,” chanzo hicho kiliongeza, kikisisitiza kuwa Hamas “inakataa mipango yoyote ya sehemu au ya muda”.
Afisa huyo alikariri kuwa Hamas inataka makubaliano ya kina ambayo ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa huko Gaza ili kubadilishana idadi iliyokubaliwa ya wafungwa wa Kipalestina, usitishaji vita wa kudumu, kujiondoa kabisa kwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza, na kuingia kwa misaada ya kibinadamu.
Kulingana na chanzo hicho, “Israel inataka kuwarejesha mateka wake katika kundi moja au mbili ili kurudisha makubaliano ya muda”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.