Chukua Hatua!

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unaweza kukosa unachotaka, kutoka kwa mtu mwingine kwa sababu ya kuhitimisha KUTOKUWEZEKANA kwa jambo, kabla hata haujachukua HATUA.

Kuna watu ambao ukiwaangalia unajua kabisa wana kitu ambacho wanaweza kukusaidia, aidha kama fursa, pesa au connection fulani.

Changamoto ya watu wengi huwa ni kuogopa “kumface” huyo mtu, kwa Imani kuwa ATAWAKATALIA.

Ukiwauliza wamejuaje kama atawakatalia, huwa wanatoa sababu za namna walivyomsikia kutoka kwa watu wengine, ama wanavyowajua watu wa namna hiyo.

Usisahau kanuni hii, USIJIAMBIE HAPANA KABLA HAUJAJARIBU.

Kuna wengi wamekosa FURSA kubwa kwa kujiambia hapana kabla hawajajaribu.

Wengine walipojaribu, walishangaa WALIKUBALIWA KIRAHISI tofauti na walivyofikiria.

Leo, amua KUJILIPUA.

Mtafute na mwambie, muombe Appointment, mpigie simu, mwandikie meseji USIKUBALI KUSHINDWA KABLA HAUJAJARIBU.

Chukua Hatua!

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment