Polisi wanatembea nyumba hadi nyumba kutafuta wazazi wa watoto waliotelekezwa kupitia DNA

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Polisi wanawasaka wazazi wa watoto watatu waliotelekezwa dakika chache baada ya kuzaliwa mashariki mwa London, na wamesema kuwa sasa wanachunguza takriban nyumba 400 zilizo karibu.

Mtoto Elsa aliachwa kwenye begi la kubebea viatu karibu na njia ya kutembea kwa miguu huko Newham mnamo 18 Januari 2024, kabla ya kugunduliwa na mtu mmoja aliyekuwa anatembea na mbwa wake.

Vipimo vya DNA alivyofanyiwa vilithibitisha kwamba alikuwa ndugu wa watoto wengine wawili, mvulana na msichana, kila mmoja akiwa amepatikana katika hali kama hiyo mnamo mwaka 2017 na 2019.

Licha ya polisi kufungua mashtaka, wazazi wa watoto hao watatu bado hawajatambuliwa.

“Walituruhusu kuwafuata maafisa waliokuwa wakienda nyumba hadi nyumba wakiwataka wakazi kutoa sampuli za DNA ili kuona ikiwa zinafanana na watoto hao,” BBC imesema.

Pia wanawasiliana na watu ambao sampuli zao za DNA zinaendana na mama huyo baada ya kupata taarifa zao kutoka kwenye hifadhidata ya kitaifa ya DNA.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment