Trump atarajia kukutana na kiongozi wa Syria baada ya kutangaza kuwa ataondoa vikwazo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ataondoa vikwazo dhidi ya Syria, kabla ya mkutano unaotarajiwa na kiongozi wake Ahmed al-Sharaa.

Trump amekubali “kukutana” na rais wa mpito wa Syria siku ya Jumatano nchini Saudi Arabia kama sehemu ya ziara yake ya Mashariki ya Kati, Ikulu ya White House ilisema.

Tangazo la kuondolewa kwa vikwazo hivyo lilipokelewa kwa shangwe katika mji mkuu wa Syria wa Damascus, ambapo nderemo, dansi na milio ya risasi ya kusherehekea ilisikika.

Vikwazo hivyo hapo awali vilizuia ufadhili wowote wa kigeni, ikiwa ni pamoja na msaada kufika Syria na awali vilikusudiwa kuweka shinikizo kwa udikteta wa Rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad.

Trump alisema mabadiliko ya sera yataipa Syria “nafasi ya ukuu”, akiambia kongamano la uwekezaji huko Riyadh ya Saudi Arabia, “ni wakati wao wa kung’aa.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al-Shaibani alisherehekea uamuzi huo kama ” mabadiliko muhimu kwa nchi” katika mahojiano na shirika la habari la nchi hiyo, Sana.

Nchi inatazamia mustakabali wa “utulivu, kujitosheleza na ujenzi wa kweli baada ya miaka mingi ya vita haribifu”, aliongeza.

Asilimia 90 ya wakazi wa Syria waliachwa chini ya kiwango cha umaskini mwishoni mwa utawala wa Assad na serikali yake mpya imekuwa ikishinikiza kuondolewa kwa vikwazo tangu Assad alipopinduliwa mwezi Disemba.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment