Sokwe warekodiwa wakitumia dawa za mitishamba ‘kujitibu’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Sokwe nchini Uganda wameonekana wakitumia dawa za mitishamba – kwa njia nyingi – kutibu majeraha ya wazi na mengineo.

Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Oxford, wakishirikiana na timu ya wenyeji katika Msitu wa Budongo, walipiga picha na kurekodi matukio ya wanyama hao wakitumia mitishamba kujipatia huduma ya kwanza, wao wenyewe na mara kwa mara kwa kila mmoja wao.

Utafiti wao unatokana na ugunduzi wa mwaka jana kwamba sokwe hutafuta na kula mimea fulani ili kujitibu.

Wanasayansi pia walikusanya miongo kadhaa ya uchunguzi wa kisayansi ili kutengeneza orodha ya njia tofauti ambazo sokwe hutumia ” dawa za mitishamba kujitibu”.

Watafiti wanasema utafiti huo, ambao umechapishwa katika jarida la Frontiers in Ecology and Evolution, unaongeza ushahidi kuwa jamii ya sokwe inayojumuisha nyani, orangutangu, tumbili na wengineo hutumia dawa za asili kwa njia tofauti ili kuwa na afya nzuri msituni.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment