Waafrika Kusini walio wazungu wawasili Marekani chini ya Mpango wa Wakimbizi wa Trump

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Kundi la Wazungu 59 wa Afrika Kusini wamewasili Marekani, ambapo watapewa hadhi ya ukimbizi.

Rais Donald Trump amesema maombi ya wakimbizi kwa Waafrika na walio wachache nchini humo yameharakishwa kwa sababu walikuwa waathiriwa wa “ubaguzi wa rangi”.

Serikali ya Afrika Kusini ilisema kundi hilo halipitii mateso yoyote ambayo yangestahili hadhi ya ukimbizi.

Utawala wa Trump umesitisha uandikishaji mwingine wote wa wakimbizi, pamoja na waombaji wengine kutoka maeneo yenye vita.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilielezea hatua hiyo kama badiliko la kikatili la ubaguzi wa rangi, likisema kuwa maelfu ya watu – wengi wao ni wakimbizi waafrika na wa Afghanistan – wamenyimwa hifadhi hiyo nchini Marekani.

Kundi la Wazungu Waafrika Kusini, ambao walitua katika uwanja wa ndege wa Dulles karibu na Washington DC siku ya Jumatatu, walipokelewa vizuri na mamlaka ya Marekani.

Wengine walishika watoto wadogo na kupeperusha bendera ndogo za Marekani katika eneo walilokuwa wamewasili.

Mchakato wa kupata hadhi ya ukimbizi nchini Marekani mara nyingi huchukua miezi na hata miaka, lakini kundi hili limefuatiliwa haraka.

UNHCR – shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi – lilithibitisha kwa BBC kuwa halikuhusika katika mchakato wa uhakiki kama ilivyo kawaida.

Alipoulizwa moja kwa moja siku ya Jumatatu kwa nini maombi ya wakimbizi wa Afrika wenye asili ya wazungu yameshughulikiwa haraka kuliko makundi mengine, Trump alisema “mauaji ya halaiki” yalikuwa yanafanyika na kwamba “wakulima wenye asili ya kizungu” walikuwa wakilengwa.

“Wakulima wazungu wanauawa, lakini ama wawe ni wazungu au waafrika hakuna tofauti yoyote kwangu.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment