Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Jitambue Wewe Ni Nani Mbele Za Mungu
ii. Wekeza Katika Maarifa
iii. Kuwa Mtatuzi Wa Matatizo
iv. Uwe Mwenye Bidii
v. Uwe Mtu Wa Kuchukua Hatua
Katiba Makala Hii Tutazungumzia Funguo Ya Kwanza
– Jitambue Wewe Ni Nani Mbele Za Mungu
Mungu anapokupa maono huwa pia anakuwa ameweka kalenda ya namna unavyoweza kuyatimiza pia.
Kuna majira na nyakati ambazo amezipanga ili kila kitu anachotaka ukifanye kiweze kutimia.
Hata hivyo kuna baadhi ya watu huwa wanachelewa.
Kuna mahali ambapo kwa sasa ulitakiwa kuwepo kulingana na ratiba ya Mungu…
…kuna mambo ulikuwa unatakiwa kuwa umeshayafanya tayari.
Shetani anaposhindwa kukuzuia, anatumia mbinu ya kukuchelewesha kufika unakokwenda kwa njia ya kuleta hali ya kufeli.
Kuleta maumivu, kusababisha ukataliwe au kuleta udhaifu ambao utakufanya ujione hauna thamani.
Maono yanapofunuliwa kwako ni kukusaidia ili uweze kukimbia nayo (Habakuki 2:2).
Kuna funguo tano ambazo watu wengi waliofanikiwa kutimiza maono yao kwa wakati na kwa kiwango kikubwa walizitumia.
Ukianza kutumia funguo hizi leo, Maisha yako yatabadilika kwa haraka sana.
Watu wengi sana kwa kutokujua wao ni nani, wamekubali kuwa wa kawaida sana…
…na matokeo yake wameshindwa kufanya mambo makubwa kwenye Maisha.
Wewe ni mtu maalumu sana mbele za MUNGU.
Hii ndio maana Mungu anasema, anajua mawazo anayokuwazia…
…ni mawazo ya kukufanikisha na kukupa tumaini kwa ajili ya siku zako za mwisho. (Yeremia 29:11).
Watu wanapokuangalia wanakuona kuwa ni mtu wa kawaida…
…ila Mungu anapokuangalia anakuona wewe ni mtu maalumu wa kipekee ambaye umetoka katika familia ya kifalme (1 Petro 2:9).
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.