Zelensky akaribisha pendekezo la Putin la kufanya “mazungumzo ya moja kwa moja” na Ukraine katikati ya mwezi huu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Zelensky

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amekaribisha wito wa Rais wa Urusi Vladimir Putin wa mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya nchi hizo mbili.

Zelensky alielezea wito wa Putin kama “ishara nzuri” inayoonesha kwamba Urusi inaanza kufikiria kumaliza vita, lakini alitoa wito tena kwa Moscow kuzingatia usitishaji wa mapigano, kuanzia Jumatatu.

Putin alitoa wito wa “mazungumzo ya moja kwa moja” na Ukraine, katika taarifa yake ya kwanza tangu kumalizika kwa mapatano ambayo Urusi ilitangaza kuadhimisha Siku ya Ushindi.

“Tunatafuta mazungumzo mazito ili kuondoa sababu kuu za mzozo huo na kuanza kuelekea kwenye amani ya kudumu,” Putin alisema katika hotuba yake iliyotangazwa kwenye televisheni ya Urusi, akitaka mazungumzo ya Istanbul kuanza “bila kuchelewa, labda mapema Mei 15.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment