Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mtangazaji wa zamani wa BBC Idhaa ya Kiswahili, Charles Hilary ameafariki dunia alfajiri ya leo Jumapili, Ikulu ya Rais Zanzibar imetangaza.
Hilary ambaye amejizolea umaarufu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa kazi yake ya utangazaji amefikwa na umauti akiwa ni Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na msemaji mkuu wa serikali ya Zanzibar.
Taarifa ya Ikulu inaeleza kuwa kifo chake kimetokea katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar Es Salaam. Taarifa kutoka kwenye familia inaeleza kuwa alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake.
Hilary alijiunga na BBC mwaka 2006 na kuwa sehemu muhimu ya timu ya watangazaji wa habari na pia kipindi cha Ulimwengu wa Soka kinachorusha matangazo ya mpira wa Ligi Kuu ya England kila wikendi.
Alikuwa pia sehemu ya watangazaji wa awali wa matangazo ya televisheni ya Dira TV mwaka 2012. Mwaka 2015 aliondoka BBC baada ya kuhudumu kwa miaka tisa na kurejea nyumbani Tanzania.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.