Waziri Mkuu wa Israel ‘hana uhakika’ juu ya hali ya mateka watatu walioko Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Waziri mkuu wa Israel amesema kuna “mashaka” kuhusu hali ya mateka watatu kati ya 24 walioaminika kuwa hai waliotekwa na Hamas huko Gaza.

Benjamin Netanyahu alisema alijua “kwa uhakika” kwamba mateka 21 walikuwa hai lakini hali ya “watatu zaidi” haijabainika wazi.

Maoni yake ameyatoa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa mateka 24 walikuwa hai wiki moja iliyopita lakini idadi hiyo sasa ilikuwa 21.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Marekani Jumanne na hakutaja chanzo wala kutoa maelezo zaidi.

Baraza la Mateka na Familia zilizotoweka lilikuwa limedai maelezo.

Jukwaa hilo pia lilimtaka Netanyahu kusitisha mipango yake ya kuongeza mashambulizi ya Israel huko Gaza na badala yake kukubaliana na Hamas kuwarejesha mateka wake 59 waliosalia na waliokufa.

Msemaji alitoa wito kwa waziri mkuu “kusimamisha vita hadi mateka wa mwisho atakaporejea”, na kuongeza: “Hili ni dharura na muhimu zaidi la kitaifa.”

Akizungumza kwenye video siku ya Jumatano kufuatia matamshi ya Trump, Netanyahu alisema: “Tunajua kwa uhakika kwamba mateka 21 wako hai. Lakini kuna wengine watatu ambao hakuna kama wako hai.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment