Vita 5 Kubwa Ambazo Kila Mkombozi Wa Familia Lazima Azishinde…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Uchungu Unaotokana na Utegemezi Wa Ndugu Wasio Na Shukrani.

ii. Ugomvi Usioisha Wewe Na Mwenzi Wako

iii. Kushindwa Kujiendeleza Kiuchumi

iv. Changamoto Ya Malezi Ya Watoto

v. Kupata Changamoto Za Kiafya

Katika Makala Hii Tutazungumzia Vita Ya Nne

– Changamoto Ya Malezi Ya Watoto

Maisha ya wakombozi wengi sana huwa hayana utulivu kabisa.

Mara nyingi maisha yao huwa yanaambatana na kusafiri na kukosa muda na familia zao.

Hii ni kwa sababu wengi hulazimika kufanya kazi kwa muda wa ziada ili kutunza familia na ndugu zao.

Na kwa sababu mara nyingi mkombozi anakuwa ameinuliwa kwenye zile njia nne nilizoelezea…

…anajikuta anakuwa bize sana na majukumu yake ya kiofisi, kwenye biashara au kukitumia kipaji chake.

Wakati mwingine mkombozi huwa analazimika kuhama hama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kama njia ya kutafuta pia.

Wakati anafanya hivi unakuta anakosa muda kabisa wa kufuatilia malezi na maendeleo ya watoto wake kitabia au kielimu pia.

Hii ndio maana unakuta watoto wengi wa wakombozi wa familia huwa wanakuwa na changamoto sana kwenye eneo la shule.

Au wakati mwingine wanakuwa na tabia zisizoeleweka.

Na wengi wanaishia kwenye matatizo ya wizi, ulevi, kuacha shule au kuzaa/kuzalisha hovyohovyo.

Wengi wanaweza kuishia kulaumu watu hawa ila wasichojua ni kuwa maisha ya mkombozi huwa yanaandamwa na…

Kutumia muda mwingi sana kwa ajili ya wengine na anaweza akajikuta anasahau watoto na familia yake.

Sura inayofuata tutajifunza namna ya kulikabili jambo hili ili lisikutokee.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment