Ukraine yasema usitishaji mapigano ya Urusi ni dhihaka

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Makubaliano ya usitishaji vita ya Urusi kwa siku tatu yameonekana kuwa dhihaka kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulizi katika uwanja wa vita, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Andrii Sybiha amesema.

Aliishutumu Urusi kwa ukiukaji mara 734 tangu mapatano yake yalipoanza kutekelezwa usiku wa kuamkia Alhamisi, akiongeza kuwa Ukraine ilikuwa ikijibu “ipasavyo” kwa kila shambulio.

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisisitiza usitishaji mapigano – ulioitishwa na Vladimir Putin kuadhimisha Siku ya Ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia – ulikuwa ukitekelezwa na kuishutumu Ukraine kwa ukiukaji mara 488.

Takriban mtu mmoja aliuawa katika mkoa wa Sumy kaskazini mwa Ukraine kufuatia shambulizi la Urusi, kulingana na huduma za dharura.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment