Njia 4 Anazotumia Mungu Kumuinua Mkombozi Wa Familia…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Njia 4 Anazotumia Mungu Kumuinua Mkombozi Wa Familia…

i. Kupitia ELIMU au UJUZI

ii. Kupitia BIASHARA

iii. Kupitia CHEO/NAFASI

iv. Kupitia KIPAJI

Katika Makala Hii Tutazungumzia Njia Ya Nne

– Kupitia KIPAJI

Mkombozi katika njia hii huibuliwa kupitia kipaji chake cha kuzaliwa nacho.

Kipaji alichonacho kinamfanyia nafasi, kinamtengenezea jina…

…na kinampa sauti kisha kinampa pesa.

Pesa ambayo inamfanya kuwa mtu muhimu kwenye familia husika.

Kwa hapa kipaji kinaweza kuwa cha kutumia Sauti kama vile muimbaji.

Au kinaweza kutumia nguvu zake kama vile mcheza mpira wa miguu.

Au kinaweza kutumia mikono yake kama vile mchoraji, mfumaji n.k.

Kwa sababu ya nguvu ya kipaji…

…mara nyingi mtu anayeinuliwa kwa njia hii huwa anakuwa amebeba jina la familia.

Na ndio hulitangaza na kulifanya lijulikane kila mahali.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment