Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moshi mweusi umeonekana ukitoka kwenye paa la Kanisa la Sistine huko Vatican, hivyo basi, ni sahihi kusema kuwa bado Papa mpya hajapatikana.

Mchakato huo unaweza kudumu kwa muda gani?
Ni muda gani ambao unaweza kuchukua kumchagua mrithi wa Papa Francis.
Mkutano wa mwisho, ambao ulimchagua Francis mnamo 2013, ulidumu kwa siku mbili na ulihusisha duru tano za kura zilizopigwa.
Mnamo mwaka 2005, wakati Papa Benedict XVI alipochaguliwa na makadinali waliokusanyika, mchakato huo pia ulidumu kwa siku mbili na kuchukua duru nne za upigaji kura kwa jumla, wakati mkutano wa kumchagua John Paul II mnamo 1978 ulichukua siku tatu na duru nane za upigaji kura zilizopigwa.
Katika mikutano ya kisasa, kumi tangu mwanzo wa karne ya 20, wastani wa muda ulikuwa siku tatu na duru saba za upigaji kura.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.