Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Manchester United wameiambia Chelsea kwamba italazimika kulipa pauni milioni 65 ili kumsajili winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Alejandro Garnacho msimu huu wa kiangazi. (Star)
Everton na Wolves wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicolas Pepe, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 29 akimaliza mkataba wake na Villarreal msimu wa kiangazi. (Foot Mercato – in French)
Winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, amebadilisha wakala wake, jambo ambalo limeweka alama ya swali kuhusu mustakabali wake katika klabu ya Bayern Munich na kuongeza mkataba ambao ulikaribia kuafikiwa. (Sky Sports in Germanty)

Beki wa kulia wa Liverpool anayeondoka Trent Alexander-Arnold yuko tayari kusaini mkataba wa miaka sita na Real Madrid ambao utaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai. (Subscription required)
Alexander-Arnold, 26, alikataa ofa ya nyongeza ya mshahara ili kusalia na Liverpool hadi mwisho wa msimu huu. (ESPN)
Liverpool wanatazamiwa kutumia pesa nyingi msimu wa kiangazi huku Reds wakitafuta beki mpya wa kushoto, beki wa kati na mshambuliaji. (Sport)

Chelsea wanatazamia kufanya mazungumzo na kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 23, kuhusu kandarasi mpya msimu huu kama zawadi kwa uchezaji wake mzuri msimu huu. (Telegraph – subscription required)
Mlindalango wa Southampton na England Aaron Ramsdale, 26, anasakwa na Manchester United na West Ham . (Mirror)

Aston Villa inamfuatilia mlinda mlango wa Real Madrid na Ukraine Andriy Lunin, 26, huku mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez, 32, akiendelea kuhusishwa na kuondoka majira ya kiangazi. ( Birmingham Mail)
Meneja wa Fulham Marco Silva na mkufunzi wa Nottingham Forest Nuno Espirito Santo ni miongoni mwa wagombea wanaowaniwa na klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal. (Sport )
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.