Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Milwaukee, Hannah Dugan, amekamatwa na maafisa nchini Marekani kwa madai ya kumsaidia mtuhumiwa wa uhamiaji kutoroka mahabusu kwa kutumia mlango wa siri wa majaji katika jengo la mahakama.
wa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Sheria ya Marekani, tukio hilo lilitokea Aprili 18,2025 wakati maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji (ICE), FBI na DEA walipofika mahakamani kumkamata Eduardo Flores-Ruiz, raia wa Mexico aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kufanya vurugu nyumbani.
Jaji Dugan anadaiwa kuwazuia maafisa hao bila kibali cha mahakama, na kumruhusu Flores-Ruiz kutoka kupitia mlango wa upande wa majaji akiwa na wakili wake.
Flores-Ruiz alikamatwa muda mfupi baadaye nje ya jengo la mahakama baada ya kufukuzwa kwa miguu na maafisa wawili waliokuwa karibu na chumba cha mahakama.
Jaji Dugan alifikishwa mahakamani siku ya Ijumaa na kusomewa mashtaka ya kuzuia utekelezaji wa sheria na kumficha mtu anayesakwa, makosa ambayo yakithibitika yanaweza kumuweka gerezani hadi miaka sita.
Wakati wa kusomewa mashtaka, wakili wake alisema Jaji Dugan “ana uchungu na anakataa vikali kukamatwa kwake,” akisisitiza kuwa hatua hiyo haikuchukuliwa kwa maslahi ya usalama wa umma.
Kwa sasa, Dugan yuko huru kwa dhamana akisubiri kusikilizwa kwa kesi hiyo Mei 15. Msemaji wake alisema, “Jaji Dugan atajitetea kwa nguvu na anatarajia kusafishwa.”
Tukio hili limezua mijadala mikali nchini humo, huku baadhi ya wanasiasa wakilitazama kama hujuma dhidi ya uhuru wa mahakama, huku wengine wakisisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.