Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov anasema Urusi “iko tayari kufikia makubaliano” na Marekani ili kumaliza vita, ingawa baadhi ya vipengee vinahitaji “kuainishwa”.
Akizungumza na shirika la habari la CBS News, ambalo ni mshirika wa habari wa BBC, Lavrov alisema: “Rais wa Marekani anaamini kwamba tunaelekea katika mwelekeo sahihi, na nadhani ni sawa, .”
Alipoulizwa kwanini ilichukua Urusi muda kufikia uamuzi huu licha ya Ukraine kusema mwezi Machi kwamba iko tayari kwa makubaliano ya usitishaji mapigano kwa maslahi ya raia wake, Lavrov alisema “tunashambulia malengo ya kijesh pekee au maeneo ya kiraia yanayotumiwa na jeshi”.
Huku hayo yakijiri, jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi ilirusha ndege 103 zisizo na rubani katika mashambulizi ya usiku kucha, ambayo yalisababisha vifo vya watu watatu.
Vifo viliripotiwa katika eneo la Pavlohrad, mashariki mwa mkoa wa Dnipropetrovsk nchini Ukraine.
Katika chapisho katika mtandao wa Telegram, Gavana wa eneo Serhiy Lysak anasema: “Mvamizi alishambulia tena eneo hilo kwa njia zisizo na rubani… mIoto kadhaa pia ulizuka huko Pavlohrad.”
Mji wa Kharkiv kaskazini-mashariki wa Ukraine pia ulishambuliwa. Kwa mujibu wa Meya Ihor Terekhov, majengo kadhaa ya kibinafsi yaliharibiwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.