Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwanafunzi mmoja ameuawa na takriban watu watatu kujeruhiwa kwa kudungwa kisu katika shule ya kibinafsi magharibi mwa Ufaransa, vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema.
Shambulio hilo lilitokea katika shule ya Notre-Dame-de-Toutes-Aides huko Nantes siku ya Alhamisi mchana, kulingana na ripoti.
Mshambulizi huyo anasemekana kukamatwa katika eneo la tukio baada ya kuzuiliwa na mwalimu.
Uwepo mkubwa wa polisi na huduma za dharura zilitumwa katika shule hiyo, ambayo wanafunz walihamishwa.
Walioshuhudia walizungumza na vyombo vya habari vya ndani na kueleza kuwa wanafunzi walikuwa wanakimbia huku na kule, huku wengine wakiwa wamefungiwa madarasani baada ya king’ora kulia.
Ouest France iliripoti kwamba wazazi walikuwa wamefahamishwa kuhusu shambulio hilo na kuwa mamlaka ilisaidia wanafunzi kuondoka pole pole.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.