Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

India imefunga kivuko chake kikuu cha mpaka na Pakistan, kuwafukuza wanadiplomasia wake na kusitisha mkataba wa kihistoria wa kugawana maji kufuatia shambulio lililoua watalii 26 huko Kashmir, jimbo linalodhibitiwa na India.
Pakistan imekana kuhusika na shambulio hilo na itaitisha mkutano wa usalama wa kitaifa siku ya Alhamisi kujadili jibu la hatua zilizochukuliwa na India.
Watu wenye silaha walitoka msituni siku ya Jumanne na kuwafyatulia risasi watalii katika shambulio hilo karibu na mji wa kitalii wa Pahalgam.
Bado hakuna uthibitisho wa ni nani aliyetekeleza shambulio hilo.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alikatisha safari yake ya nje na kurudi Delhi kukutana na wakuu wa usalama. Ameahidi waliohusika hawataachwa.
Kashmir, ambayo inadaiwa na India na Pakistan, imeshuhudia uasi wa miongo kadhaa dhidi ya utawala wa India na uasi huo umegharimu maisha maelfu ya watu – lakini mashambulizi dhidi ya watalii ni nadra.
Ripoti zinaonyesha ufyatuaji risasi ulifanyika kwa hadi dakika 20 au 30. Washambuliaji wote walifanikiwa kutoroka kabla ya vikosi vya usalama kufika kwenye eneo la tukio – operesheni ya kuwasaka imeanzishwa. Serikali ya India hadi sasa haijalaumu kundi lolote kwa kutekeleza shambulizi hilo.
Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan ilijibu shambulio hilo kwa kutoa rambirambi kwa familia za waliouawa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.