Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wakristo kutoka Afrika wanatumai mmoja wao anaweza kuwa Papa katika historia ya sasa ya kanisa hilo na kuendeleza urathi wa hayati Papa Francis wa kutetea nchi zinazoendelea, ingawa uwezekano wa hilo kutokea unaonekana kuwa mdogo.
Bara hilo ambalo dini ya kikristo imeenea katika nyanja nyingi za maisha binafsi na ya umma, ndiko ambapo Kanisa Katoliki linakua kwa kasi zaidi, kulingana na takwimu za Vatican zilizochapishwa mwezi uliopita.
Shirika la habari ya Reuters linasema, Wakatoliki kutoka Afrika waliohudhuria ibada za kumuenzi Francis baada ya kifo chake siku ya Jumatatu wamesema Papa Mweusi amechelewa kupatikana kwa muda mrefu.
“Kuwa na Papa Mweusi kunaweza kufufua imani ya Wakristo barani Afrika na kubadilisha mitazamo ya watu kuhusu Afrika, kwa kuonyesha kwamba Mwafrika anaweza kushika wadhifa huu,” amesema Charles Yapi, kasisi wa Kikatoliki katika mji mkuu wa kibiashara wa Ivory Coast, Abidjan.
Wasomi wa Kanisa Katoliki wametoa ushahidi kwamba baadhi ya Mapapa wa milenia ya kwanza walizaliwa Afrika Kaskazini au walikuwa na asili ya Afrika, ingawa maelezo juu ya historia hiyo ni machache.
Majina ya baadhi ya wagombea wa kutoka Afrika yamekuwa yakisambazwa, lakini watu kutoka ndani ya Vatican wana shaka kwamba yeyote kati yao ana nafasi ya kuwa Papa, kwa sababu hakuna hata mmoja ambaye amefanyiwa uchunguzi kama Makadinali wengi wa Magharibi.
Miongoni mwa makasisi kutoka Afrika wanaotajwa ni pamoja na Kadinali wa Ghana, Peter Kodwo Appiah Turkson, 76, Kadinali Fridolin Ambongo Besungu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, 65, Askofu mkuu wa Kinshasa, na Kadinali Ignace Bessi Dogbo wa Ivory Coast, 63.
Afrika kuna takribani 20% ya Wakatoliki wa duniani hadi mwaka 2023 na kuongeza waumini wapya milioni 9 mwaka uliotangulia.
Hata hivyo, baadhi ya makasisi wanasema maadili ya Papa ni muhimu zaidi kuliko kupata Papa kutokana na nchi au jamii atokayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.