Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mazungumzo ya London yanayolenga kupata usitishaji vita kati ya Ukraine na Urusi yapungua makali kwani hayatawajumuisha tena Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na mjumbe maalum Steve Witkoff.
Mkutano wa Jumatano badala yake utafanyika kati ya maafisa wakuu kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ukraine, na Marekani, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy atakuwa mwenyeji katika mkutano na mwenzake wa Ukraine.
Mjumbe wa Trump wa Ukraine, Jenerali Keith Kellogg, atahudhuria mazungumzo hayo badala ya Rubio na Witkoff.
Wakati huohuo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amefutilia mbali kuitambua Crimea inayokaliwa kwa mabavu kama eneo la Urusi, baada ya ripoti kupendekeza hilo linaweza kujadiliwa katika mazungumzo hayo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alisema atapanga upya safari yake ya kwenda Uingereza katika miezi ijayo. Ikulu ya White House imesema Witkoff atasafiri hadi Moscow wiki hii kwa mkutano wake wa nne na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Haya yote yanakuja huku kukiwa na ripoti katika gazeti la Financial Times kwamba Urusi iko tayari kusitisha uvamizi wake.
Katika taarifa nyignine, siku ya Jumatano asubuhi, watu tisa waliuawa katika mji wa Marhanets nchini Ukraine baada ya ndege isiyo na rubani ya Urusi kushambulia basi lililokuwa limebeba wafanyakazi.
Inakadiriwa kuwa maelfu ya watu wameuawa au kujeruhiwa kila upande tangu Urusi ilipoivamia Ukraine tarehe 24 Februari 2022, na karibu Waukraine milioni saba kwa sasa wameorodheshwa kama wakimbizi duniani kote.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.