Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kanisa la Kipentekoste nchini Afrika Kusini lilisherehekea Pasaka siku ya Jumapili kwa harusi kubwa za karibu watu 3,000, huku wengi wao wakiingia kwenye ndoa za wake wengi.
Kwa mujibu wa shrika la habari la AP, Kanisa la International Pentecost Holiness Church limesema ndoa za watu wengi ni sehemu ya sikukuu ya Pasaka na ndoa za wake wengi ambazo zinakubalika katika baadhi ya tamaduni za Kiafrika, zimeingizwa ndani ya kanisa hilo.
Sherehe ya Jumapili ilishuhudia baadhi ya wanaume wakioa wake zao wa sita au wa saba, alisema msemaji wa kanisa Vusi Ndala. Maharusi wengine walioa mke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
Kanisa la International Pentecost Holiness Church lilianzishwa nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa miaka ya 1960. Ni kanisa lililoanzishwa na Waafrika na sio wamishonari wa kigeni, na linachanganya imani za Kipentekoste na mila za wenyeji.
Kanisa hilo liliwahi kufanya harusi kubwa hapo awali, ikiwa ni pamoja na mwaka 2023 ambapo karibu watu 400 walifunga ndoa. Lakini tukio la mwaka huu ni kubwa zaidi.
Ndala amesema kuwepo kwa idadi kubwa ya watu mwaka huu ni kwa sababu ya “idadi kubwa ya wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.”
Baadhi ya mabwana harusi wameleta mke au wake zao wa sasa ili wawe pamoja nao kwa ajili ya ndoa mpya.
Harusi hizo zilifanyika katika makao makuu ya kanisa hilo, katika mji wa Heidelberg, karibu na Johannesburg, kwenye jengo linaloweza kuchukua watu 60,000.
Kuoa wake wengi ni halali nchini Afrika Kusini ikiwa ndoa hiyo imesajiliwa kama ndoa ya kimila.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.