Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Chuo kikuu cha Harvard kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya utawala wa Trump kikidai kuwa kuzuia kwake ufadhi wa serikali kwa chuo hicho wa thamani ya mabilioni ya dola ni kinyume cha sheria.
Rais wake, Alan M Garber, alitangaza hatua hiyo Jumatatu katika barua kwa jumuiya ya chuo kikuu ambayo ilisema kuzuia ufadhili wa $ 2bn kungezuia utafiti muhimu wa magonjwa.
Harvard, chuo kikuu tajiri zaidi duniani, wiki jana kilikataa orodha ya matakwa ambayo utawala wa Trump ulisema yalibuniwa kuzuia mipango yenye nia tofauti na kupiga vita chuki dhidi ya Wayahudi shuleni.
Kujibu kesi hiyo, Ikulu ya White House ilisema mpango wa kupata “pesa nyingi kupita kiasi kutoka kwa serikali” ulikuwa unafikia kikomo.
Kupunguzwa kwa ufadhili pia kumetekelezwa katika vyuo vikuu vingine, na kikosi kazi kipya cha serikali cha kupambana na Wayahudi kimetambua angalau vyuo vikuu 60 kwa ukaguzi.
Rais Donald Trump amevishutumu vyuo vikuu kwa kushindwa kuwalinda wanafunzi wa Kiyahudi wakati wa maandamano ya mwaka jana katika vyuo vikuu kupinga vita huko Gaza na uungaji mkono wa Marekani kwa Israel.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.