Dola la Kiislamu ladai kuhusika na mashambulizi mabaya nchini Nigeria

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

EW

Kundi la Dola la Kiislamu la Afrika Magharibi (ISWAP) limedai kuhusika na mfululizo wa mashambulizi mabaya yaliyolenga vikosi vya usalama vya Nigeria pamoja na raia wa Kikristo katika mikoa ya kaskazini mashariki mwa Nigeria mapema mwezi huu.

Kupitia jumbe saba zilizochapishwa kwenye shirika lake la habari la “Amaq,” ISWAP imedai ilifanya oparesheni hizi, ikiunga mkono taarifa hizo kwa video inayoonyesha moja ya mashambulio hayo na albamu mbili za picha zilizorekodi operesheni nyingine mbili.

Mashambulizi hayo katika jimbo la Borno yalilenga kambi ya jeshi la Nigeria katika mji wa Yamtage ambapo kundi hilo limedai kuwauwa wanajeshi watatu na kuteketeza kambi hiyo.

ISWAP pia imedai wapiganaji wake waliwakamata na kuwaua wanamgambo wanne wanaoiunga mkono serikali wanaojiita jeshi la Nigeria katika jimbo hilo hilo.

Katika jimbo la Adamawa, kundi hilo lilidai kuhusika na mashambulizi mawili katika kijiji cha Banga, cha jamii ya Wakristo.

La kwanza, Aprili 15, lilisababisha vifo vya Wakristo wawili na kuchomwa moto kwa zaidi ya nyumba 30 na kanisa, na “Amaq” imechapisha picha za shambulio hilo.

Shambulio la pili ni huko Banga, Aprili 16, lililenga askari polisi wa Nigeria katika kijiji hicho, na kuharibu gari na kujeruhi maafisa kadhaa.

Pia ilitoa albamu ya picha inayoonyesha shambulio katika kijiji cha Lareh huko Adamawa, ikionyesha nyumba za Wakristo na kanisa likichomwa moto.

Wapiganaji wa Boko Haram na ISWAP wamekuwa wakiendesha shughuli zao kaskazini mashariki mwa Nigeria na kulenga vikosi vya usalama na raia, na kuua au kuwafukuza maelfu ya watu.

Serikali ya Nigeria imesema itasambaratisha makundi haya, na kuongeza bajeti ya ulinzi ya mwaka huu kwa zaidi ya 40%.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment