Ukraine na Urusi zashutumiana kuvunja ‘makubaliano ya kusitisha vita wakati wa Pasaka

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ew

Ukraine na Urusi zimeshutumiana kukiuka “makubaliano ya kusitisha vita wakati wa Pasaka kwa saa 30 yaliyotangazwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumamosi, ambayo sasa muda wake umeisha.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema wanajeshi wa Urusi wamekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano karibu mara 3,000 tangu kuanza kwake siku ya Jumapili.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema “imezuia” mashambulizi ya Ukraine na kuishutumu Kyiv kwa kurusha mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora kwenda Urusi.

BBC haijathibitisha madai ya pande hizi mbili.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump – ambaye amekuwa akishinikiza kumalizika kwa vita – amesema “natumai Urusi na Ukraine zitafanya makubaliano ya kumaliza vita wiki hii,” bila kutoa maelezo zaidi.

Urusi ilifanya uvamizi mkubwa wa Ukraine tarehe 24 Februari 2022, na kwa sasa inadhibiti karibu 20% ya eneo la Ukraine, pamoja na rasi ya kusini ya Crimea iliyotwaliwa na Moscow mwaka 2014.

Inakadiriwa kuwa maelfu ya watu – wengi wao wakiwa wanajeshi – wameuawa au kujeruhiwa kila upande tangu 2022.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment