Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kupunguza ufadhili mwingine wa dola bilioni 1 kwa Chuo Kikuu cha Harvard, akilenga tafiti juu ya masuala ya afya, limeripoti Jarida la Wall Street siku ya Jumapili.
Utawala wa Trump umezuia ufadhili wa serikali kwa vyuo vya Harvard, Columbia na vyuo vikuu vingine kwa kuruhusu kwao maandamano ya wanaounga mkono Palestina katika kile ambacho utawala umesema kushindwa kudhibiti chuki dhidi ya Wayahudi kwenye vyuo vikuu.
Wiki iliyopita Harvard, ilikataa matakwa ya kudhibiti serikali yake ya wanafunzi, vitivo na mitaala, ikisema matakwao hayo yaingeifanya serikali kukidhibiti chuo hicho.
Ndani ya saa chache baada ya Harvard kuchukua msimamo huo, utawala wa Trump ulitangaza kuzuia dola bilioni 2.3 katika ufadhili wa serikali kwa chuo hicho na siku iliyofuata ulitishia kuipokonya Harvard hadhi yake ya kutolipa ushuru.
Tangu kuapishwa kwake Januari, Trump amekabiliana na vyuo vikuu vya juu vya Marekani, akisema vilishindwa kushughuliki maandamano ya mwaka jana ya kuuga mkono Gaza na kuruhusu chuki kuzidi chuoni.
Waandamanaji, ikiwa ni pamoja na baadhi ya makundi ya Kiyahudi, wanasema ukosoaji wao wa hatua za Israel huko Gaza unachanganywa kimakosa na chuki dhidi ya Wayahudi.
Orodha ya matakwa hayo kwa Harvard ili chuo hicho kiendelee kupokea ufadhili wa Shirikisho – ni pamoja na kupiga marufuku barakoa, kuondolewa sera jumuishi, sera za usawa na ushirikiano zaidi na vikosi vya usalama.
Vilevile Harvard imetakiwa kuacha kuyatambua baadhi ya makundi yanayounga mkono Palestina na kukitaka chuo hicho kuripoti kwa serikali ya shirikisho juu ya wanafunzi wa kigeni wanaokiuka sera za chuo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.