Nini kinatokea Papa anapofariki?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Nini kinatokea Papa anapofariki?

Mazishi ya papa kwa kawaida yamekuwa tukio la kipekee na lenye mambo mengi, lakini Papa Francis hivi majuzi aliidhinisha mipango ya kufanya utaratibu mzima usiwe mgumu.

Mapapa waliotangulia walizikwa katika majeneza matatu yaliyotengenezwa kwa mvinje, risasi na mwaloni.

Papa Francis amechagua jeneza rahisi la mbao lililowekwa zinki.

Pia amefutilia mbali utamaduni wa kuuweka mwili wa Papa kwenye jukwaa lililoinuliwa – linalojulikana kama ‘catafalque’ – katika kanisa la St Peter Basilica kwa ajili ya kutazamwa na umma.

Badala yake, waombolezaji wataalikwa kutoa heshima zao huku mwili wake ukisalia ndani ya jeneza, kifuniko kikiwa kimetolewa.

Francis pia atakuwa Papa wa kwanza katika zaidi ya Karne moja kuzikwa nje ya Vatican.

Atazikwa katika Basilica ya St Mary Major, mojawapo ya mabasili kuu manne ya Papa huko Roma.

Matatizo ya kiafya miezi ya mwisho ya Papa

Katika miezi ya mwisho ya maisha yake, afya yake ambayo ilikuwa imeanza kuzorotailimlazimu Papa kuwa hospitalini kwa wiki kadhaa.

Mnamo tarehe 14 Februari, Papa mwenye umri wa miaka 88 alipelekwa katika hospitali ya Gemelli huko Roma alitibiwa nimonia iliyokuwa imemuathiri katika mapafu yote mawili.

Alikuwa na matatizo ya kupumua kwa siku kadhaa.

Aliruhusiwa kutoka hospitalini mnamo Machi 23.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment