Mkuu wa Pentagon alichapisha kwenye kundi la pili taarifa nyeti juu ya mipango ya kuishambulia Yemen

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

dx
Maelezo ya picha,Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth na mkewe Jennifer Rauchet kwenye Ukumbi wa Statuary kabla ya hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth alitoa maelezo juu ya shambulio la Machi dhidi ya Waasi wa Yemen wanaosaidiwa na Iran katika kundi la ujumbe mfupi lililojumuisha mkewe, kaka yake na wakili wake binafsi, chanzo kinachofahamu suala hilo kimeiambia Reuters siku ya Jumapili.

Ufichuzi huu wa pili unaibua maswali zaidi kuhusu matumizi ya Hegseth ya mifumo fiche ya kutuma jumbe nyeti za usalama.

Suala hilo limekuja katika wakati mgumu kwake, kwani maafisa wakuu wamefukuzwa huko Pentagon wiki iliyopita kama sehemu ya uchunguzi wa ndani wa uvujaji wa taarifa.

Katika mazungumzo ya pili kwenye kundi la mtandao wa Signal, Hegseth alitoa maelezo ya shambulio sawa na yale yaliyofichuliwa mwezi uliopita na jarida la The Atlantic baada ya mhariri wake mkuu, Jeffrey Goldberg, kujumuishwa kwenye kundi la Signal kimakosa, katika tukio la aibu lililohusisha maafisa wote wakuu wa usalama wa taifa wa Rais Donald Trump.

Mtu anayefahamu suala hilo, ambaye amezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema kundi hilo linajumuisha watu kadhaa na liliundwa wakati wa mchakato wake wa uthibitisho ili kujadili maswala ya kiutawala na sio mipango ya kijeshi.

Taarifa hizo zilijumuisha maelezo ya ratiba ya mashambulizi ya anga, mtu huyo alisema.

Mke wa Hegseth, Jennifer, mtayarishaji wa zamani wa Fox News, amehudhuria mikutano nyeti na maafisa wa kijeshi wa kigeni, kulingana na picha ambazo Pentagon imezichapisha hadharani.

Wakati wa mkutano Hegseth alikuwa na mwenzake wa Uingereza huko Pentagon mwezi Machi, mke wake alionekana ameketi nyuma yake.

Msemaji wa Pentagon Sean Parnell, bila ushahidi, alisema vyombo vya habari “vinachukua malalamiko ya wafanyakazi wa zamani wenye chuki kama vyanzo vya makala zao.”

Watunga sheria wa chama cha Democratic wanataka Hegseth aondolewe kwenye wadhifa wake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment