Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

China imeonya kuwa itachukua hatu dhidi ya mataifa ambayo yanafanya makubaliano na Marekani ambayo yataathiri maslahi ya Beijing, huku vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yakitishia kuathiri mataifa mengine.
Kauli hiyo imekuja baada ya ripoti kwamba Marekani inapanga kuzishinikiza serikali kuzuia biashara na China ili kupata misamaha ya ushuru wa forodha wa Marekani.
Siku ya Jumatatu, China iliishutumu Washington kwa kutumia vibaya ushuru na kuzionya nchi nyingine dhidi ya kuingia makubaliano mapana ya kiuchumi na Marekani na kuiathiri China.
Beijing itapinga vikali nchi yoyote kuingia katika makubaliano kwa gharama ya kuathiri uchumi wa China, na “itachukua hatua za kukabiliana na hilo,” imesema Wizara yake ya Biashara.
Wizara hiyo ilikuwa ikijibu ripoti ya Bloomberg, kwamba utawala wa Trump unajiandaa kuyashinikiza mataifa yanayotaka kupunguziwa ushuru au kupara misamaha ya Marekani kuzuia biashara na China, ikiwa ni pamoja na kuweka vikwazo vya kifedha.
Katika mfululizo wa hatua za Washington, imepandisha ushuru kwa bidhaa za China hadi 145%, na kuifanya Beijing kulipiza kisasi ushuru wa 125% kwa bidhaa za Marekani. Wiki iliyopita, China iliashiria haitaongeza ushuru zaidi.
China imedhamiria na ina uwezo wa kulinda haki na maslahi yake, na inapenda kuimarisha mshikamano na pande zote, wizara hiyo ilisema.
Ikiendeleza na msimamo wake, Beijing wiki hii itaitisha mkutano usio rasmi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuishutumu Washington kwa uonevu na kuvuruga juhudi za kimataifa za amani na maendeleo” kwa kutumia ushuru.
Mapema mwezi huu, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Jamieson Greer alisema karibu nchi 50 zimemwendea ili kujadili ushuru uliowekwa na Rais Donald Trump.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.