Marekani yashambulia kituo cha mafuta cha Houthi nchini Yemen

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Jeshi la Marekani limesema limeharibu kituo cha mafuta nchini Yemen wakati wa mashambulizi yake ya hivi punde dhidi ya waasi wa Houthi.

Inasema lengo la shambulio kwenye bandari ya Bahari ya Shamu ya Ras Isa lilikuwa ni kuzuia usambazaji na fedha kwa vuguvugu hilo lenye kuungwa mkono na Iran.

Kulingana na Houthi, takriban watu 33 waliuawa wakati wa shambulio hilo na wahudumu wa dharura walikuwa miongoni mwa waliouawa.

Shambulio hilo la Alhamisi linawadia baada ya jeshi la Marekani kuongeza mashambulizi yake dhidi ya Wahouthi mwezi mmoja uliopita.

Maafisa wa Marekani hawakujibu mara moja ombi la kutoa maoni juu ya idadi ya vifo iliyotolewa na vyombo vya habari vya Houthi, shirika la habari la Reuters liliripoti.

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran walianza kushambulia meli za kibiashara katika Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden baada ya kuanza kwa vita vya Israel na Gaza mnamo Oktoba 2023.

Mashambulizi hayo yamezamisha meli na kulazimisha kampuni nyingi za meli kuacha kutumia Bahari ya Shamu – njia kuu ya biashara ya kimataifa ambayo hutumika na karibu 15% ya biashara ya baharini.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment