Hamas yakataa rasmi pendekezo la Israel la kusitisha mapigano

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Hamas imekataa rasmi pendekezo la hivi karibuni la Israel la kusitisha mapigano, ikisema iko tayari kujadili mara moja makubaliano ambayo yatahakikisha kuachiliwa kwa mateka wote waliosalia ili kumaliza vita kabisha na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina.

Katika taarifa yake kwa njia ya video, mpatanishi mkuu wa Hamas, Khalil al-Hayya, alisema: “Hatutakubali makubaliano nusu nusu ambayo yanatumikia kwa ajenda ya kisiasa ya [Waziri Mkuu wa Israel Benjamin] Netanyahu.”

Mateka hamsini na tisa bado wameshikiliwa na 24 wanadhaniwa kuwa hai. Pendekezo la hivi punde zaidi la Israel lilihusisha usitishaji mapigano wa siku 45 kwa malipo ya kuachiliwa kwa mateka 10.

Waziri wa Fedha wa Mrengo wa kulia wa Israel Bezalel Smotrich alisema ni wakati wa “kufungua milango ya kuzimu” kwa Hamas.

Maafisa wa Hamas walikuwa tayari wameashiria kwa BBC mapema wiki hii kwamba wangekataa mpango huo.

“Netanyahu na serikali yake wanatumia makubaliano ya nusu nusu kuziba ajenda zao za kisiasa, ambazo zimejikita katika kuendeleza vita vya maangamizi na njaa, hata kama itagharimu kuwatoa kafara wafungwa wake wote [mateka],” Hayya alisema.

Aliongeza kuwa kundi hilo “liko tayari kujadili mara moja makubaliano ya kubadilishana mateka wote na idadi iliyokubaliwa ya Wapalestina waliofungwa na Israel” na kumaliza vita.

Hamas hapo awali ilisema ingetafakari makubaliano ya jumla ya kumaliza vita lakini pande hizo mbili haziko karibu na aina yoyote ya makubaliano ambayo yatafanikisha hilo.

Lengo la Israel ni kuwapokonya silaha na kuwaangamiza kabisa Hamas. Wakati huohuo makumi ya raia wa Gaza wanakufa kila siku katika mashambulizi ya anga bila msaada wowote wa kibinadamu hata angalau kidogo kuingia ukanda huo.

Msururu wa hivi punde wa mashambulizi ya Israel yaliwauwa takriban watu 37, wengi wao wakiwa ni raia waliokimbia makazi yao katika kambi yenye mahema, kulingana na shirika la ulinzi wa raia wa Gaza lenye kuendeshwa na Hamas.

Mashahidi katika eneo la al-Mawasi walisema makumi ya Wapalestina wakiwemo watoto wamefariki baada ya mahema kuchomwa moto kufuatia mlipuko “mkubwa”.

Vita hivyo vilianza tarehe 7 Oktoba 2023 wakati Hamas ilipofanya mashambulizi ya kuvuka mpaka kwa jumuiya za Israel, na kuua karibu watu 1,200 na kukamata mateka 251 kulingana na hesabu za Israeli.

Kampeni ya kijeshi ya Israel dhidi ya Hamas imeua takriban watu 51,065, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment