Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Makumi ya wanachama wa bodi inayowakilisha Wayahudi nchini Uingereza wamelaani serikali ya Israel kwa “vita vya kuvunja moyo” huko Gaza.
Ni kwa mara ya kwanza kundi hilo la wayahudi katika bodi mojawapo kubwa huko Uingereza, kutoa msimamo wake wa wazi unaokosoa mashambulizi ya hivi karibuni ya Isarel huko Gaza.
Katika majibu yake uongozi wa Bodi hiyo iliyo na wanachama 300, imesema wanaelewa kuwa ni asilimia kumi tu ya washirika walioweka Saini barua hiyo.
Hata hivyo, pia wanajua wako baadhi wengine ambao huenda wana maoni kama hayo lakini wasingependa wajulikanne hadharani.
Uongozi huo umeongea kusema .., wengine pia wangependa msisitizo uwekwe kwa jinsi Hamas iendelee kuwajibishwa kwa shambulio la Oktoba 7 ili kuondoa uwezekano wowote wa tukio kama hilo kurudiwa.
Walioweka saini barua hiyo wameeleza kinaga ubaga hofu zao hususan kuhusu ‘mustakbali wa baadae wa Israel’.
‘’Serikali ya Israel imechagua kuendeleza vita badala ya kutumia njia za kidiplomasia kufanya makubaliano ya awamu ya pili ya jinsi ya kupata suluhu la kudumu. Israel imetamaushwa na mashambulizi hayo na sisi kama wanachama wa bodi hii ya wayahudi huku Uingereza tuna hofu ya itakavyokuwa Israel ya baadae… taifa tunalolipenda na tulilonalo uhusiano wa karibu.’’
Tangu tarehe mbili mwezi jana Israel kwa mara nyingine tena imezuia misaada ya vyakula na dawa za matibabu kuingia Gaza, huku wakizidisha mashambulio wanayosema wanalenga kutokomeza kundi la Hamas lakini pia yanaishia kuwauwa raia wengi wasio na hatia ikiwemo watoto.
Hamas imeishtumu Israel kwa kuvunja mkataba wa kusitisha vita ambao ulikuwa uingie katika awamu ya pili. Ni katika awamu hii ambapo ilitarajiwa ingepelekea makubaliano ya jinsi mateka wote wangeachiwa huru na kupatikana suluhu la kudumu la kusitishwa kwa mapigano.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.