Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Man Utd inamtaka kipa Ramsdale

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bournemouth wamekubali kuwa wataachana na beki wa Kihispania Dean Huijsen msimu huu wa joto, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anapendelea kuhamia klabu nyingine ya ligi kuu England badala ya Bayern Munich au Real Madrid. (Talksport)

Manchester United wanamfuatilia kipa wa Southampton Aaron Ramsdale, mwenye umri wa miaka 26, kufuatia wasiwasi kuhusu kiwango cha kipa wa Kimataifa wa Cameroon Andre Onana, mwenye umri wa miaka 29. (The Sun)

Manchester United wana wawafuatilia angalau makipa wanne, wakiwemo Bart Verbruggen wa Brighton, kipa wa Kiholanzi mwenye umri wa miaka 22. (i paper)

Chelsea wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Brighton, Georginio Rutter, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (Florian Plettenberg)

.
Maelezo ya picha,Thomas Partey

Atletico Madrid wanapanga kumsajili tena kiungo wa Arsenal Thomas Partey, mwenye umri wa miaka 31, msimu huu wa joto. (Marca – in Spanish)

West Ham wanataka kumsajili kipa wa Liverpool Caoimhin Kelleher, mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha la usajili la majira ya joto. (Daily Mirror)

Newcastle wamewapiku Real Madrid na Barcelona katika kumsaini winga wa Malaga mwenye umri wa miaka 18, Antonio Cordero. (Fabrizio Romano)

Aston Villa wanapiga hatua katika mazungumzo na Rosenborg kuhusu kiungo wa kati wa Norway mwenye umri wa miaka 18, Sverre Halseth Nypan. (Sky Sports)

Tammy Abraham
Maelezo ya picha,Tammy Abraham

AC Milan na Roma watafanya usajili wa kudumu wa mshambuliaji wa Kiingereza Tammy Abraham, 27, na kiungo wa Ubelgiji Alexis Saelemaekers, 25, licha ya hali ya kutokuwa na uhakika wa makocha katika vilabu hivyo. (Corriere dello Sport – in Italian)

Kocha wa Newcastle Eddie Howe ameiambia bodi ya klabu hiyo kuwa anataka kuendelea kuwa na wachezaji wake bora msimu huu wa joto, wakiwemo mshambuliaji wa Uswidi mwenye umri wa miaka 25, Alexander Isak, ambaye anahusishwa na Liverpool na Arsenal. (Teamtalk)

Kipa wa Kiingereza Tom Heaton, 39, na beki wa Kaskazini mwa Ireland mwenye uzoefu Jonny Evans, 37, wanatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu wa joto baada ya mikataba yao kuisha. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Ipswich Town Liam Delap, 22, atakataa uhamisho kwenda Manchester United msimu huu wa joto. (Daily Star)

.
Maelezo ya picha,Jurgen Klopp

Aliyekuwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, ambaye sasa ni mkuu wa soka wa kimataifa katika Red Bull, anaibuka kama chaguo la kumrithi Carlo Ancelotti katika Real Madrid. (Sport – in Spanish)

Tottenham wamewatambua Marco Silva wa Fulham, Thomas Frank wa Brentford na Andoni Iraola wa Bournemouth kama wagombea wa nafasi ya kumrithi Ange Postecoglou iwapo atatimuliwa. (Teamtalk)

Iraola huenda akakataa nafasi ya kujiunga na Tottenham na kubaki Bournemouth, huku Cherries wakilenga kucheza soka la Ulaya msimu ujao. (Telegraph – subscription required)

Aliyekuwa kocha wa Sevilla na Argentina Jorge Sampaoli yuko katika mazungumzo ya kuwa kocha mpya wa klabu ya Neymar ya Brazil, Santos. (TNT Sports)

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment