Mwanamke anafasiriwa kwa jinsia ya kuzaliwa- Mahakama

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

GG

Mahakama Kuu ya Uingereza imeamua kwamba mwanamke, kwa mujibu wa sheria, ni mtu aliyezaliwa akiwa na jinsia ya kike.

Majaji wamesema kuwa jinsia ni ya aina mbili tu—mwanaume au mwanamke—na kwamba uamuzi huu haupaswi kuchukuliwa kama ushindi wa upande wowote.

Mahakama pia imeeleza kuwa watu waliobadili jinsia bado wanalindwa kisheria dhidi ya ubaguzi.

Uamuzi huu umetolewa baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya serikali ya Scotland na kundi la wanawake la For Women Scotland.

Serikali ya Scotland ilikuwa ikitaka watu waliobadili jinsia( transgender) na wana cheti cha utambuzi wa jinsia (GRC) wahesabiwe katika kundi linalopata ulinzi wa kijinsia.

Lakini kundi la For Women Scotland walipinga, wakisema ulinzi huo unapaswa kutolewa kwa waliozaliwa wanawake pekee.

Uamuzi huu unaweza kuathiri sheria na sera katika Scotland, England na Wales.

Baada ya uamuzi huo, Susan Smith kutoka shirika la For Women Scotland alisema: “Wanasiasa wanapaswa kuelewa kuwa huu ndiyo uamuzi wa sheria. Ni lazima waache kutoa mwongozo usio sahihi kwa shule na hospitali. Hii bado ni vita inayoendelea,” alisema.

Katika uamuzi wa ukurasa 88 wanawake wameeleza kuwa mahakama kuu imeainisha vizuri sheria ya usawa.

Haya yakijiri mwandishi wa Berlin- kuhusu malezi na mhadhiri Ravna Marin Nathanael Siever anasema kuamua kutomuita mtoto msichana au mvulana ni jambo ambalo lilianza kupata umaarufu katika miaka 1980, hasa katika jamii za watu ambao hawamini kuwa wako katika jinsia yoyote ile(queer).

Hii iliambatana na kile wanachokielezea kama “wimbi la pili la utetezi wa jinsia ya kike”, huku wanawake wengi wakipinga kuitwa kama wasaidizi wa nyumbani au katika kazi za aina fulani.

Malazi ya wazazi ya usawa katika jinsia, yalijitokeza sio kuweka usawa wa jinsia za watoto, “bali kuwaruhusu kugundua utambulisho wao wao wenyewe, kuliko kuambiwa utambulisho wao na watu wengine”, anasema Siever.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment