Mchungaji wa Marekani aliyetekwa nyara wakati wa ibada huko aokolewa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mchungaji wa Marekani ambaye alitekwa nyara na watu wenye silaha wakati wa ibada ya kanisani nchini Afrika Kusini wiki jana ameokolewa kufuatia “mapigano makali ya risasi” yaliyosababisha vifo vya watu watatu, mamlaka zimesema.

Josh Sullivan alipatikana akiwa hana jeraha katika kitongoji cha Gqeberha eneo la Cape Mashariki Jumanne jioni – ambalo mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 45 alitekwa nyara Alhamisi iliyopita.

Hakukuwa na maelezo ya haraka juu ya watekaji nyara ambao wanashukiwa kufahamu mienendo ya familia hiyo.

Katika kipindi cha muongo uliopita, kumekuwa na ongezeko la asilimia 264 la utekaji nyara nchini Afrika Kusini, kulingana na takwimu za polisi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment