Urusi imehukumu mfungwa wa kivita aliyejisalimisha kwa Ukraine – vyombo vya habari

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mahakama ya kijeshi ya Yuzhno-Sakhalinsk Garrison limekamilisha kusikiliza kesi ya kwanza ya jinai juu ya kujisalimisha kwa hiari wakati wa operesheni za kijeshi nchini Ukraine, gazeti la Kommersant limesema.

Chanzo cha gazeti hilo kilisema kwamba Jumanne, Roman Ivanishin, mfungwa wa kivita kutoka kitengo cha 39 wa Walinzi wa Brigedi ya Rifle, alihukumiwa kifungo cha miaka 16 chini ya ulinzi mkali.

Kulingana na gazeti hilo, mtu huyo alipatikana na hatia ya kujisalimisha, jaribio lingine la kujisalimisha na kwamba aliacha kitengo chake cha jeshi.

Awali, Gazeti la Kommersant liliandika, Ivanishin alifanya kazi kama msimamizi katika mchimbo ya madini huko Sakhalin, na “aliishia kwenye Jeshi wakati wa usajili wa wanajeshi wa akiba.”

Baada ya mafunzo ya muda mfupi, kitengo chake kilitumwa katika eneo lililojitangia uhuru la DPR iliyojitangaza, ambapo alitekwa na vikosi vya jeshi la Kiukreni mnamo Juni 10, 2023.

Akiwa ameshikwa na jeshi la Ukraine, video ilirekodiwa ambpo alitoa wito kwa wanajeshi wengine wa Urusi kutoroka kutoka kwa vitengo vyao.

Mwanzoni mwa Januari 2024, alirejeshwa katika mabadilishano ya wafungwa wa vita vya Ukraine, na kesi ya jinai ilifunguliwa dhidi yake nchini mwake.

Hata hivyo, Ivanishin amekanusha kuwa na hatia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment