Njia 7 Za Kukabili Vikwazo Vinavyowazuia Wanawake Wengi Kusonga Mbele…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kukata Tamaa Kwasababu Ya Mambo Yaliyopita.

ii. Dependency Syndrome

iii. Kukosa Kujiamini (Lack of Self-belief)

iv. Emotional Instability (Kukosa Uimara wa Kihisia)

v. Kutokusamehe

vi. Kuambatana na Watu Wasio Sahihi (Wrong Association)

vii. Kutokuwa na Mpango wa Mafanikio ya Kifedha

Katika Makala Hii Tutazungumzia Njia Ya Tano

– Kutosamehe

Moja ya ushauri muhimu sana ambao niliwahi kusikia kwa mfanyabiashara maarufu sana Mwamerika mweusi aliyefanikiwa, Oprah Winfrey, ni pale aliposema:

“Learn to Forgive and Let it go” (Jifunze kusamehe na kuachilia).

Maneno haya aliyazungumza baada ya kuulizwa aliwezaje kuanza upya katika maisha yake baada ya kupitia manyanyaso mengi yakiwemo kubakwa zaidi ya mara moja na ndugu wa karibu, kupata mtoto akiwa na umri mdogo na mengine mengi.

Ushauri wake ulikuwa:

“Jifunze kusamehe na kuachilia.”

Watu wengi sana ambao wameumizwa huu si ushauri rahisi sana, na mara nyingi wakipewa ushauri huu wanasema:

“Ni kwa sababu hujui namna nilivyoumizwa.”

Maumivu ya kutokusamehe yamesababisha uchungu kwa watu wengi sana, na matokeo yake yamewafanya kushindwa kabisa kuchukua hatua inayofuata.

Ni ukweli usiopingika kwamba kuna maumivu makali sana ambayo umeyapitia na mengine hayaelezeki, ni kweli yameacha vidonda vikubwa sana katika maisha yako.

Lakini ukweli mwingine ambao ni lazima uukubali ni kuwa, kusamehe na kuachilia ni njia moja ya kupata uponyaji wa kudumu ili usonge mbele.

Watu wengi sana wanapofikiria suala la kusamehe na kuachilia huwa wanaona kama vile watawapa faida wale ambao wamewakosea.

Kwa kawaida ungependa waje kwako na wakuombe msamaha na uridhishe nafsi yako.

Kitu ambacho unatakiwa kujua ni kuwa sababu ya kwanza ya kuwasamehe ni kwa faida yako na sio si faida yao.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment