Trump: Nitafanya uamuzi kuhusu Iran hivi karibuni

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba anatarajia kutoa uamuzi kuhusu Iran hivi karibuni.

Maoni hayo yanajiri baada ya nchi zote mbili kuripoti mazungumzo “chanya” na “ya kujenga” huko Oman siku ya Jumamosi na kukubaliana kuanza tena mazungumzo wiki hii.

Trump, ambaye hapo awali alitishia kuchukua hatua za kijeshi ikiwa makubaliano ya kuzuia mpango wa nyuklia wa Iran hayatafikiwa, aliwaambia waandishi wa habari ndani ya Air Force One Jumapili usiku, saa za Mashariki, kwamba amekutana na washauri wake kuhusu Iran na anatarajiwa kufanya uamuzi hivi karibuni, Hakutoa maelezo zaidi.

Haya ni maoni mafupi ya pili ya Bw. Trump tangu mazungumzo na Abbas Araqchi na Steve Whittaker siku ya Jumamosi.

Lakini Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei hadi sasa hajatoa tamko lake Katika maoni yake ya kwanza kwa waandishi wa habari, Trump alikuwa amesema: “Nadhani mazungumzo yanaendelea vyema.

Hakuna muhimu kusema hadi yatakapokamilika. Kwa hivyo sipendi kulizungumzia. Lakini sio mabaya.

Nadhani yanakwenda vizuri kiasi. Katika mkutano na makamanda wa kijeshi siku ya Jumapili, Ayatollah Khamenei alisisitiza kwamba lazima wawe na “maandalizi ya hali ya juu na tahadhari za vifaa na programu.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment