Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Arsenal kumnunua winga wa Real Madrid Arda Guler kwa £35m

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.
Maelezo ya picha,Arda Guler

13 Aprili 2025

Arsenal wanapanga kuweka dau la pauni milioni 35 kumnunua winga wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 20 Arda Guler. (The Sun – Subscription Required}

Chelsea wana nia ya kumsajili beki wa Bournemouth Dean Huijsen, 19, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa timu nyingine kadhaa za Premier League. (The Athletic – Subscription Required),

Chelsea pia wanahusishwa na winga wa Real Betis mwenye umri wa miaka 19 Jesus Rodriguez, ambaye analindwa na kipengele cha kutolewa cha thamani ya hadi £42m. (Mail)

Manchester United imeongeza hamu ya kumnunua mlinda lango wa Parma Zion Suzuki, 22, huku timu hiyo ya Serie A ikimthamini mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan kwa pauni milioni 40. (Sport)

.
Maelezo ya picha,Zion Suzuki

Real Madrid wako tayari kumruhusu kiungo mkongwe Luka Modric, 39, kuondoka klabuni hapo msimu huu wa joto. (Diario AS – In Spanish)

Inter Miami wako tayari kumpa mkataba mpya mshindi mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or Lionel Messi, 38, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu. (Mirror)

RB Leipzig wana nia ya kumteua kiungo wa zamani wa Arsenal na Uhispania Cesc Fabregas, ambaye kwa sasa anainoa Como, kama meneja wao mpya. (Calciomercato – In Itali),

Manchester City, Bayern Munich na Borussia Dortmund zote zinamtaka kiungo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16 Guille Fernandez huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania chini ya umri wa miaka 19 akichoshwa na ukosefu wa nafasi katika kikosi cha kwanza katika klabu hiyo ya Catalan. (Mundo Deportivo – In Spanish)

.
Maelezo ya picha,Federico Chiesa

Liverpool wangedai ada ya kati ya £17m hadi £22m (euro 25m hadi 30m) kwa fowadi wa Italia Federico Chiesa, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akilengwa na AC Milan na vilabu vingine kwenye Premier League. (Caughtoffside)

Mkurugenzi mkuu wa Bayer Leverkusen Fernando Carro ana imani kocha Xabi Alonso na kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 21, watasalia katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sky Sports Ujerumani – In Germany)

Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa rasmi kwa kiungo wa Atalanta Ederson, 25, huku klabu hiyo ya Serie A ikimthamini Mbrazil huyo kwa takriban £52m. (Tuttomercato – In Itali)

Liverpool wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Inter Milan Nicolo Barella, 28. (Fichajes)

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment