Gabon: Mkuu wa jeshi Oligui Nguema ameshinda uchaguzi wa urais.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiongozi wa kijeshi nchinik Gabon, Brice Oligui Nguema, amepata ushindi mkubwa kufuatia uchaguzi mkuu wa rais uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, matokeo ya awali yakionesha amepata asilimia 90.35 ya kura zote.

rais uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, matokeo ya awali yakionesha amepata asilimia 90.35 ya kura zote.

Imechapishwa: 14/04/2025

Brice Oligui Nguema baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais nchini Gabon  (Photo by Daniel BELOUMOU OLOMO / AFP)
Brice Oligui Nguema baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais nchini Gabon (Photo by Daniel BELOUMOU OLOMO / AFP) © Daniel Beloumou Olomo / AFP

Nguema, ambaye alimaliza utawala wa zaidi ya miongo mitano wa utawala wa familia ya Bongo mwezi Agosti mwaka 2023 aliahidi kurejesha utawala wa kiraia.

Awali, Wizara ya mambo ya ndani ilikuwa imetangaza kuwa, mwanajeshi huyo alikuwa amefaulu kupata kura zaidi ya laki 5 ambazo zilikuwa sawa na asilimia 90.3.

Aidha wizara hiyo ilithibitisha kuwa asilimia 70.4 ya wapiga walishiriki ambapo watu Milioni 2.3 walikuwa wameandikishwa.

Oligui, ambaye alimaliza utawala wa zaidi ya miongo mitano ya utawala wa familia ya Bongo mwezi Agosti mwaka wa 2023 alikuwa ameahidi kurejesha utawala wa kiraia kwenye taifa hilo
Oligui, ambaye alimaliza utawala wa zaidi ya miongo mitano ya utawala wa familia ya Bongo mwezi Agosti mwaka wa 2023 alikuwa ameahidi kurejesha utawala wa kiraia kwenye taifa hilo REUTERS – Luc Gnago

Mpizani wake mkuu Alain-Claude Bilie By Nze, aliyehudumu kama waziri mkuu wakati wa utawala wa Ali Bongo, alipata asilimia tatu ya kura zote wakati wagombea wengine sita wakishindwa kufikisha zaidi ya asilimia moja. 

Oligui Nguema kwa sasa anatarajiwa kuapishwa ambapo ataongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka saba, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa njia ya simu alimpongeza kwa ushindi wake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment