Rais Daniel Chapo kuwasaidia wachimbaji madini wa Msumbiji wanaozuiliwa nchini Afrika Kusini

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais mpya wa Msumbiji, Daniel Chapo

Rais mpya wa Msumbiji, Daniel Chapo, kwamba amejitolea kuhakikisha kuwa raia 1,000 wa Msumbiji wanaozuiliwa nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za uchimbaji madini haramu, wameachiliwa huru.

Rais Chapo amesema kuwa lengo la utawala wake ni kuboresha hali ya uchimbaji madini wa ndani ili kuwazuia vijana wa Msumbiji kuvuka kuingia Afrika Kusini na kuhatarisha maisha yao katika operesheni hatari na zisizo halali.

Alisema ipo haja ya kuzingatia makubaliano ya kihistoria ya kazi kati ya mataifa hayo mawili, akiongeza kuwa serikali yake itaunga mkono tu taratibu za kisheria za uchimbaji madini.

Mzozo mbaya kati ya mamlaka ya Afrika Kusini na wachimba migodi haramu walionaswa katika mgodi uliotelekezwa huko Stilfontein umesababisha vifo vya watu 70 huku wachimbaji madini haramu 1,500, wengi wao wakiwa raia wa Msumbiji kukamatwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment