Kipenga Cha Michezo-Haaland asaini mkataba mpya Man City

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Erling Haaland
Maelezo ya picha,Erling Haaland ameshinda mataji mawili ya Ligi ya Premia, moja la FA na moja la Ligi ya Mabingwa tangu ajiunge na Manchester City

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland ametia saini mkataba mpya utakaomuwezesha kusalia katika uwanja wa Etihad hadi 2034.

Raia huyo wa Norway alijiunga na City akitokea Dortmund mwaka 2022 na amefunga mabao 111 katika mechi 126 aliyoichezea klabu hiyo tangu wakati huo.

Mkataba wa awali wa mshambuliaji huyo, ambao inasemekana ulijumuisha kipengele cha kumuwezesha kuhama, ulikuwa unamalizika mwaka 2027.

Mkataba mpya wa Haaland utamfanya mshambuliaji huyo kusalia na City hadi siku yake ya kuzaliwa ya 34 iwapo ataamua kusalia katika klabu hiyo hadi utakapokamilika katika muda wa miaka tisa na nusu.

“Nina furaha sana kusaini mkataba wangu mpya na ninatazamia kuwa kwa muda zaidi katika klabu hii kubwa,” alisema Haaland.

“Manchester City ni klabu maalum, iliyojaa wachezaji mahiri na wafuasi wa ajabu na ni mazingira ambayo humsaidia kila mtu kufikia ubora wake. “Pia namshukuru [kocha] Pep [Guardiola], wakufunzi wake, wachezaji wenzangu na kila mtu katika klabu hii kwani wote wamenisaidia sana katika miaka michache iliyopita.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment