Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Tanzania imesema kuwa sampuli zilizochukuliwa hazijathibitisha uwepo wa virusi vya Marburg, hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya.
“Mpaka leo tarehe 15 Januari 2025, majibu ya uchunguzi wa kimaabara…hayajathibitisha uwepo wa virusi vya Marburg”.
Hayo yanawadia baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kusema kuwa mlipuko unaoshukiwa kuwa wa virusi vya ugonjwa wa Marburg umewaua watu wanane katika mkoa wa Kagera Kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Wizara hiyo ilithibitisha kupokea tetesi za uwepo wa ugonjwa huo na kusema kuwa imechukua hatua za haraka.
“Tumetuma timu ya wataalamu; kufanya uchunguzi wa suala hili; kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara”, taarifa ya Waziri wa Afya Jenista Mhagama imesema.
Wizara hiyo imehakikishia wananchi pamoja na jumuiya ya kimataifa kuwa imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na kwamba itaendelea kutoa taarifa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.