Sudan: UN yaonya dhidi ya mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya raia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya raia wa kawaida katika jimbo la Al-Jazira nchini Sudan.

Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali ya Sudan kuhusiana na suala la uongozi.
Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali ya Sudan kuhusiana na suala la uongozi. REUTERS – Umit Bektas

Onyo hili limekuja baada ya wiki hii jeshi la Sudan ambalo limeendelea kupambana na wanamgambo wa RSF kuwafanikiwa kudhibiti tena mji mkuu wa jimbo hilo Wad Madani, baada ya mapigano makali.

Umoja wa Mataifa kupitia tume inayoshughulikia masuala ya kibinadamu inasema, machafuko dhidi ya raia wa kawaida, hayakubaliki na ni kinyume cha sheria za Kimataifa.

Mapigano nchini Sudan yamesababisha maelfu ya watu kupoteza makazi yao.
Mapigano nchini Sudan yamesababisha maelfu ya watu kupoteza makazi yao. AFP – –

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameripoti kuwa mashambulio yanayoendelea katika jimbo la Al-Jazira, yamesababisha vifo vya watu 13 wakiwemo watoto wawili.

Wanamgambo wa RSF wameendelea kushtumiwa kwa kuwalenga watu kwa sababu ya kabila wanaotokea hasa katika jimbo la Darfur, vita ambavyo vimesababisha maafa ya maelfu ya watu tangu Aprili mwaka 2023.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment